MALINDI, KIPANGA NA KILIMANI CITY NANI ATAUNGANA NA TIMU 5 KUSHUKA DARAJA
Zikiwa zimesalia mechi 2 kwa kila timu kati ya timu tatu
zilizo katika vita ya kuepuka kushuka daraja ni wazi Ligi Kuu ya Zanzibar kanda
ya Unguja msimu huu ina ushindani mwingine mkubwa chini ya msimamo kuliko
katika mbio za kutinga 8 bora, JKU, Jang’ombe
Boys na Taifa ya Jang’ombe wameshajihakikishia kutinga hatua hiyo huku
ikisubiriwa Zimamoto au Polisi ambapo Zimamoto inapewa nafasi kubwa kufuzu 8
bora.
Homa kubwa ipo kwa vilabu vitatu ambavyo ni Malindi, Kipanga
na Kilimani City na mmoja kati ya hao wataungana na vilabu vyengine vitano
ambavyo tayari vishajihakikishia kushuka daraja.
Timu 5 ambazo tayari zishajihakikishia kushuka daraja ni
Kimbunga, Chaka Stars, Miembeni, Kijichi na Mundu ambapo wanaisubiri timu moja
ili ziwe 6 kuungana kushuka daraja.
MALINDI
Malindi imebakisha michezo 2 baada ya kucheza michezo 32 hadi
sasa na kati ya michezo iliyosalia upande wao watacheza kesho kutwa Jumatano
3/5 dhidi ya KMKM saa 8:00 Amaan na
mwengine watamalizana na Taifa ya Jang’ombe ambao watacheza Jumamosi 06-05-2017
saa10:00 Amaan.
Malindi ipo nafasi ya 13 wana alama 39 katika michezo 32
waliyocheza wameshinda 11 sare 6 na kupoteza 15.
KIPANGA
Timu hii inamilikiwa
na Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambapo wamebakiwa na michezo miwili kati yao n KVZ
utakaochezwa kesho kutwa Jumatano 3/5/2017
saa 10:00 Amaan, na mchezo wao wa mwisho
watamalizana na KMKM Jumapili ya 07-05-2017 saa 1:00 USIKU Aman.
Katika Msimamo wapo nafasi ya 12 wakiwa na alama 41 kati ya
michezo 32 waliyocheza wameshinda 12, sare 5 na wamefungwa 15.
KILIMANI CITY
Kilimani City wenyewe wanajita watoto wa Mjini wamebakiwa na
michezo 2 , mmoja watacheza kesho Jumanne 02/5/2017 dhidi ya Jang’ombe Boys saa
1:00 usiku Amaan, na wa mwisho watamalizana na Chuoni Tarehe 05-05-2017 saa
1:00 za usiku Amaan.
Comments
Post a Comment