MASHABIKI,WACHEZAJI NA UONGOZI WA TAIFA YA JANG’OMBE KUKUTANA KESHO KUPANGA MIPANGO YAO YA MAENDELEO
Baada ya leo kumaliza michezo yake yote 34 ya ligi kuu soka
ya Zanzibar kanda ya Unguja timu ya Taifa ya Jang’ombe kesho watakutana
Mashabiki, Wapenzi, Wachezaji na Viongozi wao ili kujadili mambo mbali kwa
kujipanga katika hatua ya 8 bora ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Mkutano huo utafanyika kesho Jumapili Mei 7, 2017 kuanzia saa
4:00 za asubuhi katika Ukumbi wa SACCOS uliopo Meli nne mkabala na Shule ya
Mbarali.
Moja ya mambo yatakayopangwa na kujadiliwa kesho ni kuendesha zoezi la uuzaji wa kadi za uanachama wa timu hiyo ili mshabiki awe na kadi maalum ambapo fomu za kujiunga na unachama huo fomu hiyo itauzwa Shilingi Elfu 10 kisha muombaji atarejesha pamoja na picha za passport size mbili.
Katibu wa timu hiyo Mohammed Maulid “Edi Sada” amesema Mkutano huo ni muhimu kwa wote Mashabiki, Wanachama, Wachezaji na Uongozi wao ili kupanga mikakati mbali mbali ya kuitengeneza timu yao.
|
Comments
Post a Comment