MASHINDANO YA RIADHA YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI YASUKUMWA MBELE, ZANZIBAR WASEMA WATAZIDI KUJIPANGA UPYA
Chama cha Riadha Zanzibar kimepokea barua ya kutoka
Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) kwa kupelekwa mbele Mashindano ya Riadha kwa
Vijana U-17 ya Afrika Mashariki na Kati ambayo yalikuwa yafanyike kesho na
kesho kutwa Jijini Dar es salam.
Katibu wa Riadha Zanzibar Suleiman Ame amethibitisha kupokea
taarifa hiyo kutoka kwa RT ambapo amesema Mashindano hayo yamesogezwa mbele
mpaka Mei 13-14, 2017 jijini Dar es salam.
“Tumepokea Barua kutoka kwa RT kuwa mashindano yamesogezwa
mbele, lakini sisi tutazidi kujipanga mana mazoezi tunaendelea kufanya asubuhi
na jioni katika uwanja wa Amaan, sasa kusogezwa mbele inaweza kutusaidia zaidi
kufanya vizuri sisi kama Zanzibar”. Alisema Ame.
Mpaka sasa nchi tano tu zimeshathibitisha kushiriki
Mashindano hayo katika nchi 11 wanachama wakiwemo wenyeji Tanzania Bara,
Zanzibar, Kenya, Uganda na Sudani ya Kusini.
Wachezaji wa Riadha Zanzibar mwaka jana waliporejea nyumbani katika Mashindano ya Vijana |
Comments
Post a Comment