MCHAMBUZI MAARUFU WA MICHEZO ZANZIBAR HUSSEIN AHMADA ATEULIWA KUWA AFISA HABARI MPYA WA NEGRO
![]() |
Hussein Ahmada kulia, kushoto Ali Salum Rais wa Negro |
Uongozi wa klabu ya Negro inayoshiriki ligi daraja la Pili
Taifa umemteua Hussein Ahmada Vuai kuwa Afisa Habari na Mawasiliano mpya wa klabu
hiyo kuanzia jana Mei 13, 2017.
Hussein anachukua nafasi ya Awadh Haji “Machochoki” aliyehamishwa
kwenda kuwa Msemaji wa klabu ya Gereji iliyopanda Daraja la Pili Wilaya ya
Mjini ambazo zote ni timu za Jimbo la Kwahani.
Akizungumza kuhusu uteuzi huo Rais wa Negro Ali Salum “Kirova”
ambae pia ni Muwakilishi wa Jimbo la Kwahani amesema wamemchagua Hussein kuwa
Afisa Habari wao mpya kwasababu ya utendaji kazi wake na kumuona kuwa atafaa
kuisaidia na kuisemea Negro.
“Tumemteuwa Hussein Ahmada kuwa Afisa Habari wetu, Hussein ni
mchapa kazi na tumemuona kuwa atakuwa mtu sahihi kwetu, kwanza Negro ni klabu
yake ambayo anaipenda kwa vile ipo nyumbani kwao nay eye kalelewa na Negro,
mimi naamini ni chaguo sahihi na Hussein atatutangaza vizuri na kutusemea klabu
yetu”.
Kwa upande wake Hussein Ahmada ameushukuru Uongozi wa Negro
kwa kumteuwa yeye na pia kasisitiza ushirikiano kwao pamoja na Wanahabari.
“Mimi niseme kuwa hii ni fursa azimu kuipata, nawashukuru
Negro, kubwa ushirikiano kwa sote Uongozi wangu lakini hata nyinyi Waandishi wa
Habari, ntakuwa pamoja na kuhakikisha Negro inajulikanwa Zanzibar nzima na nje ya
Zanzibar”. Alisema Hussein.
Hussein Ahmada ni miongoni mwa Wachambuzi wanaofanya vizuri
sana katika Uchambuzi wa Michezo ambapo kazi hiyo ya Uchambuzi anaifanyia
kwenye kituo cha Radio cha Coconut FM kupitia kipindi cha Coco sports na pia
huwa mualikwa kwenye vituo mbali mbali vya TV kama vile Tifu TV na ZBC TV.
Comments
Post a Comment