MLANDEGE NA GULIONI HAPATOSHI KESHO
Kesho kutakuwa na Dabi kati ya Gulioni dhidi ya Mlandege kwenye mchezo wa ligi daraja la pili Wilaya ya Mjini hatua ya 4 bora mzunguko wa pili mchezo utakaochezwa saa 1:00 za usiku katika uwanja wa Amaan.
Mlandege walifungwa 1-0 na Gulioni walipokutana katika hatua ya 8 bora ambapo bao pekee la Gulioni lilifungwa na Mussa Haji Mussa, hivyo mchezo wa kesho utakuwa na upinzani mkubwa kutokana na Mlandege kutaka kulipa kisasi na Gulioni kutaka kuendelea kutunza heshima.
Katika ligi hiyo timu zote 4 Kwerekwe City, Amani Fresh, Mlandege na Gulioni zina alama 1 kufuatia mchezo wa awali City kwenda sare ya 1-1 na Gulioni, Mlandege nae akatoka sare ya 1-1 na Amani Fresh.
Mchezo mwengine utapigwa Jumatano ya Mei 10, 2017 kati ya Kwerekwe City dhidi ya Amaan Fresh.
Comments
Post a Comment