MLANDEGE YAFUFUA MATUMAINI YA KWENDA MABINGWA WILAYA
Timu ya Mlandege jana usiku imefanikiwa kuongoza katika hatua
ya 4 bora ligi daraja la Pili Wilaya Mjini baada ya kushinda mabao 3-1 dhidi ya
Gulioni mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Amaan.
Mabao ya Mlandege yamefungwa na Mohd Abdallah "Edo"
dakika ya 47 na 66 na jengine likimalizwa na Hassan Ramadhan dakika ya 68.
Bao pekee la Gulioni limefungwa na Shaabani Hassan dakika ya
28.
Kwa matokeo hayo Mlandege anaongoza akiwa na alama 4 kwa michezo miwili huku Amani Fresh
na Kwerekwe City wakiwa na alama 1 kwa mchezo mmoja mmoja wakati Gulioni wana
point 1 kwa michezo 2.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho Jumatano kwa kupigwa mchezo
mmoja katika Uwanja wa Amaan majira ya saa 10 za jioni kati ya Kwerekwe City
dhidi ya Amaan Fresh.
Bingwa na Makamo Bingwa katika ligi hiyo watawakilisha Wilaya
ya Mjini kwenda kucheza na Wilaya nyengine sita zikiwemo Magharibi “A”,
Magharibi “B”, Kaskazini “A”, Kaskazini “B”, Kati na Wilaya ya Kusini kwa
kucheza ligi ya Mabingwa wa Wilaya ambayo itakuwa na timu 14 huku timu 4
zikitafutwa kupanda Daraja la Pili Taifa Msimu ujao.
Comments
Post a Comment