NYERERE, KOCHA CHOLO NA MKENYA WASHINDA TUNZO ZA MWEZI WA APRIL, ZPL
Kamati ya ufundi ya Unguja imetangaza majina matatu ya Kocha
bora, Mchezaji bora na Muamuzi bora wa
Mwezi wa April katika ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja.
Kamati hiyo imemteua Kocha Nassor Salum wa Polisi kuwa kocha bora wa mwezi, huku Mshambuliaji wa Kipanga Daudi Nyerere katangazwa kuwa Mchezaji bora wa Mwezi na Ali Haji "Mkenya" kafanikiwa kuwa muamuzi bora wa mwezi huo.
![]() |
David Nyerere mshambuliaji wa Kipanga
Zawadi zao zitatolewa leo kwenye pambano la saa kumi uwanja wa Amaan kati ya Kipanga dhidi ya KMKM.
|
Hongera sana Kocha Cholo.usiridhike na hapo ongeza juhud we wanna see at another high level
ReplyDelete