RIKODI MUHIMU ZA TAIFA YA JANG’OMBE NA JANG’OMBE BOYS USO KWA USO KABLA MCHEZO WA LEO
![]() |
Kikosi cha Taifa ya Jang'ombe |
Timu ya
Jang’ombe Boys inarikodi nzuri ya kumtesa Taifa ya Jang’ombe baada ya kukutana
mara 6 ambapo Boys ameshinda mara 3 huku Taifa akishinda mara 2 na mchezo mmoja
kwenda sare.
Wawili hao
wote kutoka Mtaa mmoja wa Jang’ombe watakutana tena leo majira ya saa 2:00 za
usiku katika Uwanja wa Amaan kwenye mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua
ya 8 bora.
![]() |
Kikosi cha Jang'ombe Boys |
RIKODI USO KWA USO BOYS V/S TAIFA
WAMEKUTANA MARA 6 MPAKA SASA
Msimu wa mwaka 2012-2013
Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini Taifa 1-2 Boys.
Ligi ya Waamuzi dakika 90 Taifa 0-0 Boys, Penalti Taifa 4-5 Boys.
Novemba 19, 2016
Bonanza la Coconut FM Taifa 2-0 Boys.
Mabao yalifungwa na Mkongo Baraka Ushindi na Mkenya Mohd Said “Mess.
Disemba 10, 2016
Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja Mzunguko wa kwanza Taifa 2-2 Boys.
Mabao ya Taifa siku hiyo alifunga Omar Yussuf Chande dakika 9 na Abdallah Mudhihir (Mido) dakika 60 wakati mabao ya Boys yote alifunga Khamis Mussa (Rais) dakika ya 45 na 53.
Disemba 30, 2016
Kombe la Mapinduzi 2017 Taifa 1-0 Boys
Bao pekee lililofungwa na Hassan Seif “Banda”.
April 25, 2017
Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja mzunguko wa pili Taifa ya Jang’ombe 0-1 Jang’ombe Boys.
Bao pekee limefungwa na Khamis Mussa (Rais).
Comments
Post a Comment