TAIFA WAITAIFUTIA DAWA BOYS BAADA YA LEO KUFANYA MKUTANO MAALUM, HATUA YA 8 BORA WATAANZA KUKUTANA JUMAPILI HII DABI NYENGINE HIYO YA JAN’GOMBE
![]() |
Wachezaji na Mashabiki wa Taif |
Mashabiki, Wapenzi, Wachezaji na Viongozi wa timu ya Taifa ya
Jang’ombe wamekutana kwa pamoja asubuhi ya leo kwa kujadili mambo mbali katika
hatua ya 8 bora ambayo inatarajiwa kuanza wiki ijayo huku wakipania kutwaa
ubingwa wa ligi kuu soka ya Zanzibar.
Mkutano huo umefanyika leo Jumapili Mei 7, 2017 kuanzia saa
4:00 za asubuhi katika Ukumbi wa SACCOS uliopo Meli nne mkabala na Shule ya
Mbarali ambapo wamejadili mambo mengi ikiwa kujipanga katika hatua ya 8 bora
ambapo mchezo wao wa kwanza Taifa watacheza na ndugu zao Jang’ombe Boys katika
Uwanja wa Amaan saa 2:00 za usiku Jumapili ya Mei 14, 2017.
Katika Mkutano huo uliwapa fursa Wapenzi na Wachezaji
kuchangia mawazo tofauti ili timu hiyo ifanye vizuri na kutimiza lengo lao la
kubeba ubingwa wa Zanzibar.
“Lengo la Mkutano huu ni katika mpango wa kuzidi kuiboresha
timu yetu tufanye vizuri katika hatua ya 8 bora na kubeba ubingwa wa Zanzibar”.
Alisema Abdul kadir Gharib “Chabala” Meneja wa Taifa ya Jang’ombe.
Comments
Post a Comment