TAIFA WAMCHAGUA MWANASHERIA MAARUFU ZANZIBAR
Wakili msomi wa kujitegemea Omar Mmadi Mwarabu amechaguliwa
kuwa Mwanasheria wa klabu ya Taifa ya Jang'ombe.
Akithibitisha taarifa hizo Katibu wa Taifa Mohammed Maulid
"Edi Sada" amesema kutokana na soka la sasa linavyokwenda
wamelazimika kumchagua Mwarabu kuwa Mwanasheria wao ambae ataongoza mambo yote
ya kisheria yanayohusu klabu yao.
“Uongozi wa Taifa tumemteuwa Omar Mmadi kuwa mwanasheria wetu
na atasimamia na kulinda haki zote za wachezaji, haki za timu na mambo yote ya
kisheria kwa timu yetu ya Taifa”. Alisema Mohammed.
Kwa upande wake Mwanasheria huyo Omar Mmadi Mwarabu amepokea
kwa furaha sana kuteuliwa kwenye timu hiyo kuwa Mwanasheria na anaimani kuwa
haki zote za Taifa kwasasa hazitopotea tena baada ya uteuzi wake.
“Nimefurahi kuchaguliwa kuwa Mwanasheria, najua Uongozi wa
Taifa wananijua kuwa mimi ni Taifa damu damu, nawaahidi haki zote za Taifa
ntazilinda na kuzisimamia ipasavyo”. Alisema Mwarabu.
Comments
Post a Comment