TIMU YA KISANDU YATOKA SARE WAKIWA PUNGUFU WACHEZAJI 2, KESHO MECHI 7 KUPIGWA NYENGINE


Na: Fatma Suleiman, Zanzibar.

Timu ya Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar “ZJMMC” inayofundishwa na kocha Abubakar Khatib “Kisandu” jana ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Chuo cha Afya Mbweni katika Mashindano ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar “ZAHILFE CUP” uliopigwa majira ya saa 10 za jioni katika Uwanja wa Amaan.

 Mchezo huo ni wa Kundi D ambapo ZJMMC walimaliza wakiwa pungufu wachezaji wawili baada ya Walinzi wao kuonyeshwa kadi nyekundu Nassor Cholo na Said Shaha katika dakika 54 ya mchezo na 67, mchezo ambao umesimamiwa na Muamuzi mwenye beji ya FIFA Mgaza Ali Kinduli.
Timu hizo zilikwenda mapumziko wakiwa suluhu pacha, huku mchezo ukiwa na kasi ya kawaida na kosa kosa ndogo, ambapo mabao yote yalipatikana kipindi cha pili kwa Penalty kwa kila upande ambapo la Afya lilifungwa na Lucho wakati la ZJMMC lilipigwa na Omar Habibu.

Mashindano hayo  yataendelea tena kesho kwa kupigwa michezo tofauti katika viwanja tofauti.


Chuo cha Habari ZJMMC watasukumana na MCC Saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Fuoni, SUZA v/s ZU Uwanja wa SUMAIT Saa 10:00,  MNMA v/s MICROTECH uwanja wa ZU Tunguu saa 10:00 jioni, KARUME v/s ICPS Uwanja wa Polisi Ziwani saa 10:00 jioni, ZITOD v/s SUMAIT Uwanja wa SUMAIT Chukwani saa 10:00 za jioni, IPA v/s ZSH uwanja wa Amaan saa 8:00 mchana na KATI v/s ZIFA Uwanja wa Fuoni Saa 8:00 za mchana.

Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE