UCHAGUZI WA SQUACH UNAENDELEA ZIWANI POLISI
Zoezi la Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Ukuta Zanzibar “Zanzibar Squash Racket Association (ZSRA)”
linaendelea muda huu asubuhi ya leo Jumamosi Mei 6, 2017 katika Ukumbi wa
Squach wa Polisi Ziwani.
Uchaguzi huo ambao unagombewa nafasi 6 zikiwemo Mwenyekiti,
Makamo Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mshika Fedha na Mshika Fedha
Msaidizi.
Katika Uchaguzi huo hakuna hata nafasi moja iliyopata
upinzani katika nafasi sita zinazogombewa ambapo nafasi ya Mwenyekiti
itagombewa na Abuza Salim huku nafasi ya Makamo Mwenyekiti akijitokeza Nassor
Salum, nafasi ya katibu amejitokeza Mohd Hamza
na naibu katibu yupo Omar Yussuf huku nafasi ya Mshika Fedha inagombewa na
Mwanamama Fatma Saleh wakati Iddi Khamis nae akiwa pekee katika nafasi ya Mshika Fedha Msaidizi.
![]() |
Kamati ya Uchaguzi inayoongozwa na Mwenyekiti Abdallah Juma wa kati kati
Kamati itakayosimamia Uchaguzi huo ina wajumbe 7 wakiongozwa na Mwenyekiti Abdallah Juma na Katibu Yussuf Mohd Ali “Kareka” huku wajumbe wakiwa Juma Mussa Rashid, Omar Makungu Omar, Mwanaidi Abdallah Makame, Zuhura Mohd Ali na Hadia Yahya Khamis.
Kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho kila baada ya miaka 4 hufanyika Uchaguzi wa kuchagua viongozi wapya ambapo Uchaguzi uliopita ulifanyika mwaka 2012.
|
![]() |
Wadau na wachezaji wa mchezo wa Squach |
Comments
Post a Comment