WAAMUZI WATAKASIMAMIA LIGI KUU ZENJ KITUO CHA PEMBA HAWA HAPA

CHAMA cha mpira wa miguu ZFA Taifa Pemba, kimewachaguwa wamuzi watano
watano wamuzi wasaidizi sita na wasimamizi wa mchezo watatu watakao
weza kusimamia ligi kuu ya Zanzibar kwa upande wa Kisiwa cha Pemba.

Akizungumza na mwandishi wa Mtandao huu,  Mkufunzi wa Waamumuzi
Kisiwani hapa, mwamuzi mstaafu wa Kimataifa (FIFA) Ali Juma Salum,
alisema ZFA imeawachaguwa waamuzi hao kutokana na uzoefu walionao
katika kuchezesha mpira wa miguu.

Aliwataja wa Wamuzi watakao chezesha katika ligi hiyo, Suleiman Khatib
(Kisauti), Assa Ali, Mohamed Seif, Makame Haji Chirau  na  Said Ali.
Waamuzi wasaidizi ni Mwadini Ali Mwadini, Shehe Suleiman Hamoud,
Suleiman Juma (Viringi), Khalifan Ali, Tahir Silima na Shaibu Mahadhi,
wasimamizi wa michezo ni Ali Juma Salum,  Sarhani Said na  Ali Said
Ali.

“Nimewapa mafunzo kwa muda mrefu namini watayatumia ipasavyo mafunzo
yao, imani yangu ligi hii itanza vizuri na itamaliza kwa usalama
nitahakikisha kila timu itapata haki yake na sitopendelea upande
wowote”, Alisema.

Hata hivyo aliwataka viongozi wa timu, kuachana na tabiya ya
malalamiko yasiokuwa ya msingi, kwani viongozi wengi hupenda kuwalaumu
wamuzi jambo ambalo husababisha vurugu, ila  wakigundiuwa kunatatizo
wafuate taratibu na kanuni za ZFA.

Aidha aliwata mashabiki wa mipira wa miguuu, kuchana na tabia ya
kuwatukana Wamuzi, kwani wao wamechaguliwa kihali na ZFA, matusi
hupelekea  uvunjifu wa amani bali wawe na ustahamili, Wamuzi ni
binaamu kama binaadamu wengine.


Na: Abd Suleiman, Pemba.

Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE