WAMKUMBUKA ABDUL SATAR BOSS WA MLANDEGE, ARUDI TENA KATIKA SOKA NA KUELEZEA KILICHOMREJESHA NI CAF
![]() |
Abdul Satar wa kati kati alovaa kanzu nyeupe |
Najua kama wewe ni mmoja kati ya wapenda soka, Zanzibar na Tanzania nzima basi jina la Meneja wa
zamani wa timu ya Mlandege Abdul Satar litakuwa sio geni masikioni mwako.
Satar ambae tumeanza kumuona tena kwenye soka mwishoni mwa msimu huu wa mwaka 2016-2017.
Satar kwasasa amerejea tena kwenye soka akiwa tena na klabu yake ya Mlandege ambayo kwasasa inayoshiriki ligi daraja la pili Wilaya ya mjini Unguja ambapo ameelezea sababu kubwa iliyomfanya arudi tena kwenye soka baada ya kupotea zaidi ya miaka 10 sasa.
Amesema kitendo cha Zanzibar kupatiwa uanachama wa kudumu na shirikisho la soka barani Afrika “CAF” ndicho kulichompelekea yeye kurudi katika timu ya Mlandege.
“Sasa rasmi nimerudi kwenye soka ndani ya klabu yangu ya Mlandege, sababu kubwa iliyonifanya nirudi tena ni baada ya kuona ZFA imepatiwa uanachama wa kudumu na Shirikisho la soka Afrika, kitendo hichi kimenifurahisha mno ndipo nimeamua kurejea tena huku pia nawaambia Mashabiki wa Mlandege hatutosimama mpaka ligi kuu sasa, mana sisi watu wa mpira tumerejea kwenye mapenzi yetu”. Alisema Satar.
Comments
Post a Comment