ZIMAMOTO NA OKAPI ZAANZA VYEMA LIGI KUU ZENJ, KESHO HOMA YA JIJI TAIFA NA BOYS
![]() |
Kikosi cha Zimamoto |
Timu ya Zimamoto na Okapi zimefanikiwa kuanza vyema ligi kuu
soka ya Zanzibar hatua ya 8 Bora baada ya kushinda michezo yao ya leo.
Zimamoto imeifunga JKU 1-0 mchezo uliopigwa jioni ya leo
katika uwanja wa Amaan.
Bao pekee la Zimamoto limefungwa na Hassan Haji dakika ya 35.
Mchezo mwengine umechezwa jioni uwanja wa Gombani ambapo
Okapi ikaichapa Kizimbani mabao 2-1.
Kizimbani ndio wa mwanzo kupata bao kupitia Khatib Hassan
dakika ya 57, lakini Okapi wakasawazisha kupitia Nadir Mohd dakika ya 75 na
Seif Saleh dakika ya 82 kupiga bao la pili.
Kesho Jumapili ya Mei 14 itaendelea tena kwa kupigwa mchezo
kati ya Mwenge dhidi ya Jamhuri saa 10:00 za jioni katika Uwanja wa Gombani
huku Amani Mjini Unguja kutakuwa na homa ya Jiji la Jang’ombe kati ya Taifa ya
Jang’ombe dhidi ya Boys saa 2:00 za usiku.
![]() |
Kikosi cha JKU |
RATIBA KAMILI MZUNGUKO WA KWANZA
Jumapili 14/5/2017 Mwenge v/s Jamhuri, saa 10:00 Gombani.
Jumapili14/5/2017 Taifa ya Jang’ombe v/s Jang’ombe Boys, saa 2:00 usiku Amaan.
MZUNGUKO WA PILI
Jumatano 17/5/2017 Zimamoto v/s Jang’ombe Boys, saa 10:00 Amani.
Jumatano 17/5/2017 Kizimbani v/s Mwenge, saa 10:00 Gombani.
Alhamis 18/5/2017 Taifa ya Jang’ombe v/s JKU, saa 10:00 Amaan.
Alhamis 18/5/2017 Jamhuri v/s Okapi, saa 10:00 Gombani.
MZUNGUKO WA TATU
Jumapili 21/5/2017 Jang’ombe Boys v/s JKU, saa 10:00 Amaan.
Jumapili 21/5/2017 Mwenge v/s Okapi, saa 10:00 Gombani.
Jumatatu 22/5/2017 Zimamoto v/s Taifa Jang’ombe, saa 10:00 Amaan.
Jumatatu 22/5/2017 Jamhuri v/s Kizimbani, saa 10:00 Gombani.
Baada ya hapo ligi hiyo itasimama na kupisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambapo itakuja kuendelea Mzunguko wa nne mpaka imalizike Mwezi huo wa Ramadhan.
Comments
Post a Comment