ZIMAMOTO YAKAMILISHA IDADI YA TIMU 8 ZILIZOFUZU 8 BORA
ZIMAMOTO YAKAMILISHA IDADI YA TIMU 8 ZILIZOFUZU 8 BORA
Timu ya Zimamoto imefanikiwa kutinga hatua ya 8 bora kwenye
ligi kuu soka ya Zanzibar wakiwa na mchezo mmoja mkononi baada ya kupata
ushindi mchana wa leo wa mabao 6-2 dhidi ya Chwaka Stars mchezo uliopigwa
katika uwanja wa Amaan.
Mabao ya Zimamoto yamefungwa na Hassan haji dakika ya 1,48,65, Yussuf Ramadhan dakika ya 27, Idrisa Simai dakika ya 45 na Nyange Othman dakika ya 56.
Mabao ya Chwaka yamefungwa na
Ali Bai dakika ya12 na
Abdul latif Mzee dakika ya 80.
Timu nyengine zilizofanikiwa kutinga hatua hiyo ni JKU, Jang’ombe
Boys, Taifa ya Jang’ombe na Zimamoto
ambapo kwa upande wa Pemba ni Jamhuri, Mwenge, Kizimbani na
Okapi zote kutoka mkoa wa kaskazini Pemba.
Hatua ya 8 bora ndio inayotowa Bingwa na Makamo Bingwa ambao
watawakilisha Zanzibar katika Mashindano ya Kimataifa ya Klabu Bingwa na Kombe
la Shirikisho Barani Afrika.
Hatua hiyo inatarajiwa kuanza punde tu itakapomalizika ligi
zinazoendelea kwa Kanda zote za Pemba na Unguja ambazo zinatarajiwa kumalizika
Mei 7, 2017.
![]() |
Kikosi cha Zimamoto |
Comments
Post a Comment