ZU NA CHUO CHA HABARI CHA KISANDU KESHO ROBO FAINALI ZAHILFE CUP
Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar (ZAHILFE CUP) Timu ya Chuo Kikuu cha Zanzibar University (ZU) kesho watachuana na Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar (ZJMMC) katika hatua ya robo fainali kwenye Mashindano ya ZAHILFE, mchezo ambao utasukumwa saa 7:00 za mchana katika Uwanja wa Amaan.
ZJMMC ambao wanafundishwa na kocha machachari Abubakar Khatib Kisandu kesho wana kazi ngumu kupigana na ZU ambao wanafundishwa na kocha Juma Yussuf Sumbu.
Michezo mengine kesho ya robo fainali itapigwa saa 8:00 za mchana kwenye uwanja wa ZU Tunguu kati ya SUMAIT Chukwani dhidi ya IPA.
Robo fainali nyengine ya tatu itapigwa pia kesho saa 10:00 za jioni katika uwanja wa ZU Tunguu kati ya MICROTECH dhidi ya Afya Mbweni, na katika Uwanja wa SUMAIT Chukwani watakipiga chuo cha Chwaka ZIFA watasukumana na ICPS.
Comments
Post a Comment