ZU YAFUNDISHWA SOKA NA WATOTO WA MJINI WA KOCHA KING



Mohammed Seif "King" kocha wa Mjini

Mabingwa wa watetezi wa Mashindano ya Soka ya Vyuo Vikuu vya Zanzibar “ZAHILFE CUP” Chuo cha Zanzibar Univeristy jioni ya leo wamefundishwa soka na Vijana wa Kombain ya Wilaya ya Mjini baada ya kukubali kufungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa katika uwanja wao ZU Tunguu.

Bao pekee la Mjini limefungwa na Abdul hamid Juma “Samatta” ambapo ZU walishindwa kuamini kilichowakuta mbele ya Vijana hao.


Mjini wanajiandaa na Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone yatayotarajiwa kufanyika Arusha mwezi July, 2017 wakati ZU wapo katika maandalizi makali kujiandaa na Mashindano ya Vyuo Vikuu vya na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar “ZAHILFE” ambayo yanatarajiwa kuanza Jumapili hii ya Mei 14, 2017 ambapo ZU watafungua dhidi ya Chuo cha Nyerere saa10:00 za jioni katika Uwanja wa Amaan.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS