KAMA KAWAIDA YAO UNGUJA NA LEO MECHI YA 5 MFULULIZO WASHINDA, LAKINI YAHARIBU RIKODI YAKE YA KUTOTINGISHWA NYAVU ZAO, SASA WANA POINT 15 MABAO 15, JIONI WANACHEZA TENA MECHI NYENGINE LEO LEO
![]() |
Kikosi cha Unguja
Leo timu ya soka ya Unguja imeendelea kucheza mchezo wake
mwengine na kufanikiwa kushinda mabao 2-1 dhidi ya Iringa, mchezo uliopigwa saa
2 za asubuhi katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza kwenye
mashindano ya UMISSETA.
Mabao ya Unguja leo yamefungwa na Iliyasa Suleiman na Mundhir
Abdallah.
Ukiachia mchezo huo wa asubuhi pia Unguja leo jioni saa 10
watacheza mchezo wao wa mwisho wa kundi C dhidi ya timu ya Dar es salam ambao
wao leo asubuhi hawajacheza wakati wenzao Unguja watacheza michezo 2 mfululizo
kwa siku moja.
bado Unguja ndio kinara akiwa na alama 15, wakifukuzwa na Dar
es salam wenye alama 13 wote wameshacheza michezo 5 na lakini timu zote hizo
mbili zimeshakata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali.
Unguja wapo kundi “C” lenye jumla ya timu 7 ambapo wapo
pamoja na Katavi, Kagera, Mara, Mbeya, Iringa na Dar es salam.
Michezo mitano ya awali Unguja waliifunga Katavi 4-0,
wakaichapa Kagera 3-0, juzi wakaipiga Mara 5-0, jana waituguwa Mbeya 1-0, na
leo wakaipiga Iringa 2-1, hivyo wameshafunga jumla ya mabao 15 katika michezo 5
waliyocheza wakati lango lao limeruhusu kufungwa bao moja tu.
|
Nasema tena Zanzibar Vipaji vipo tatizo kuendelezwa FA na Walimu na wasimamizi wa timu tujiangalie sana nahisi tunajiona ni viongozi wa mpira kumbe ni wauwaji wa vipaji.
ReplyDelete