NINJA WA YANGA APOKELEWA KISHUJAA NA TAIFA YA JANG’OMBE
![]() |
Mlinzi mpya wa klabu ya Yanga aliyesajiliwa jana Abdallah
Haji Shaibu "Ninja" amepokelewa kwa shangwe na mamia ya mashabiki
wake punde tu alipowasili Visiwani Zanzibar mchana wa leo akitokea Jijini Dar
es salam ambako alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.
Mashabiki hao walianza kumpokea tangu Bandarini Malindi na
kumpandisha gari aina ya Canter hadi nyumbani kwao Jang’ombe huku njiani
wakimuimbia nyimbo na kupiga dufu kuashiria furaha ya mpendwa wao huyo kusajiliwa
Yanga.
Rais wa Mashabiki wa Taifa ya Jang’ombe Ismail Ibrahim “Aili”
aliongoza msafara huo ambao ulikuwa na furaha ya aina yake.
Ninja jana amesajiliwa Yanga akitokea timu ya Taifa ya
Jang’ombe inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar.
|
![]() |
Ninja akisaini jana mbele ya katibu wa Yanga Mkwasa |
Comments
Post a Comment