CHARAWE WAKANUSHA KUUZA DARAJA, WASEMA HATA WAPEWE MILIONI 200 TIMU HAWAITOWI LENGO LAO KUCHEZA LIGI KUU NA KUCHUKUA UBINGWA

Uongozi wa klabu ya Charawe Stars umekanusha taarifa za kuuza daraja kwa timu yao na kusema kuwa taarifa hizo si kweli na wao wapo katika maandalizi ya kucheza ligi kuu soka ya Zanzibar msimu ujao.

Akizungumza na Mtandao huu  Ramadhan Abdallah “Sadifa” ambae ni msemaji wa timu hiyo amesema taarifa zilizozagaa mitaani ya kuwa timu yao imeuzwa sio kweli na kamwe hawawezi kufanya jambo hilo kwani ile ni timu ya Kijiji na lengo lao kucheza ligi kuu ndio mana wakapigana kufika hapo walipo.

“Hizo taarifa sio kweli timu yetu hatuuzi wala haitouzwa, sisi tupo kwaajili ya kupambana kucheza ligi kuu ya Zanzibar, tunashukuru tumefanikiwa kutoka daraja la kwanza na kufika hapo tulipo kwasasa tunasubiri ligi kuu kucheza, hiyo timu inayosema inataka kununuwa nafsi yetu hata watuletee million 200 hatukubali, sisi tumepigana ndo mana tukafika ligi kuu na wao kama rahisi wapigane, sisi sio genge hii ni timu ya Wanakijiji, kama rahisi nawao wapigane wafike hapa tulipofika sisi, msimamo wetu timu hatuitowi hata waje na pesa gani tunataka kucheza ligi kuu ya Zanzibar na kubeba kombe” Alisema Sadifa.


Hivi karibuni kumeibuka tetesi nyingi zinazosema timu ya Mlandege SC wamenunuwa daraja la Charawe hivyo taarifa hizo za kukanusa msemaji wa Charawe zitawasaidia kujua watu wengi ambao waliyofikiria kuwa kweli timu ya Charawe imeuzwa.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS