GULIONI YAANZA MAANDALIZI MAPEMA MSIMU MPYA, SIKUKUU YA IDDI KUCHEZA NA TAIFA YA JANG’OMBE
![]() |
Kikosi cha Gulioni msimu ulopita 2016-2017 |
Timu ya Gulioni itaanza rasmi mazoezi siku ya Jumatatu ya
June 12, 2017 kwa kujiandaa na msimu wa ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini wa
mwaka 2017/2018.
Akizungumza na Mtandao huu Rais wa klabu ya Gulioni Ahmed
Khamis amesema wamepania kuanza mapema mazoezi ili msimu huu wajipange
kupandisha daraja timu yao.
Mbali na kuanza mazoezi hayo, Ahmed amesema pia wanatarajia
kucheza michezo mbali mbali ya kirafiki ukiwemo mchezo wao dhidi ya Taifa ya
Jang’ombe katika Bonanza maalum ambalo litafanyika katika sherehe za Sikukuu ya
Iddi Pili katika Uwanja wa Amaan.
“Tunatarajia kuanza mazoezi Jumatatu, tunaanza mapema
kwasababu tujiandae zaidi kuipandisha timu yetu, pia tutacheza na Taifa ya Jang’ombe
Iddi Pili kwenye Bonanza maalum”. Alisema Ahmed.
Msimu ulopita wa mwaka 2016-2017 Gulioni ilifanikiwa kutinga
katika hatua ya 4 bora ya Ligi daraja la Pili Wilaya hiyo lakini walishindwa
kusonga mbele na kulazimika kusalia katika daraja la Pili Wilaya ya Mjini.
![]() |
Wachezaji wa Gulioni wa msimu ulopita 2016-2017 |
Comments
Post a Comment