HAWA UNGUJA NOWMA HUKO MWANZA, KILA SIKU WANAWAPIGA WENZAO NYINGI, LEO WAMCHAPA MTU 5-0
Kikosi cha Unguja 2017 UMISSETA Mwanza |
Wakicheza mchezo wa tatu Timu ya soka ya Unguja imeendelea
kuwapa raha wana Mwanza kufuatia ushindi wake wa tatu mfululizo baada ya asubuhi
ya leo kuwapiga timu ya Mara mabao 5-0 kwenye Mashindano ya Michezo na Sanaa ya
Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA) katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba
mkoani Mwanza.
Mabao ya Unguja yamefungwa na Ali Hassan “Ndimbo” (2), Walid
Abdi “Pato”, Faki Kombo na Mundhir Abdallah “Diarra”.
Kwa matokeo hayo Unguja ndio kinara akiwa na alama 9 wapo
kundi “C” lenye jumla ya timu 7 ambapo wapo pamoja na Katavi, Kagera, Mara,
Mbeya, Iringa na Dar es salam.
Mchezo mwengine Unguja watacheza kesho Jumapili June 11, 2017
saa 12:30 za asubuhi dhidi ya Mbeya, kisha Jumatatu June 12, 2017 Unguja dhidi
ya Iringa, Jumanne June 13, 2017 Unguja watamalizana na Dar es salam.
Michezo mitatu ya awali Unguja waliifunga Katavi 4-0,
wakaichapa Kagera 3-0 na leo wakaipiga Mara 5-0, hivyo wameshafunga jumla ya mabao
12 katika michezo 3 wakati lango lao bado halijaonjwa hata bao moja.
Comments
Post a Comment