HILIKA AWAPA SOMO WACHEZAJI WA UNGUJA WATAKAOKWENDA UMISSETA MWANZA
Mshambuliaji wa klabu ya Zimamoto ya Zanzibar Ibrahim Hamad
Hilika amewataka wachezaji wa timu ya soka Kanda ya Unguja UMISSETA kujituma zaidi ili kufikia
malengo yao waliyojiwekea.
Hilika ameyasema hayo Amani asubuhi ya leo wakati Wachezaji
hao walipomaliza mazoezi ambapo amewapa elimu kubwa kuhusu soka ili wafanikiwe
na watimize ndoto zao.
Amewataka kujituma katika Mashindano ya UMISSETA huko Mwanza
na wacheze kwa malengo kwani Zanzibar kuna vipaji vingi sana.
“Munakwenda Mwanza ndugu zangu fursa kubwa sana mumepata,
angalieni kuna wachezaji wangapi hawajachaguliwa mumechaguliwa nyinyi, hivyo
mujuwe kuwa nyinyi mumeaminiwa mukapigane na mukaoneshe vipaji vyenu kwani sisi
Zanzibar tunavipaji vingi sana, mpira sasa ni ajira, mfano mimi nina mke wangu
na kazi yangu nimepata kwaajili ya mpira, nauthamini na naupenda kwa vile ndio
kazi yangu, ningekuwa sijajituma kucheza mpira si ningekuwa pengine sina lolote
nakaa masikani tu, sasa nyinyi kachezeni kwa kufata mafunzo na ushauri wa
walimu wenu, kwasababu nidhamu ndio siri ya mafanikio, wekeni malengo soka ni
ajira sasa, si mumesikia kuwa Zanzibar imepata uanachama wa CAF!, sasa fursa
hizo jamani, mimi nipo pamoja na nyinyi ndugu zangu, tutakufatilieni na
tutafurahi sana mukibeba ubingwa, nakutakieni safari njema yenye mafanikio”.
Alisema Hilika.
Mashindano ya UMISSETA yanayotarajiwa kuanza June 6, 2017
huko Chuo cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza ambapo kwa mwaka huu Zanzibar
itashiriki kanda mbili tofauti, yani Kanda ya Unguja na Kanda ya Pemba.
Wachezaji 21 waliyochaguliwa kwenye kikosi hicho kinachotarajiwa
kuondoka Visiwani Zanzibar siku ya Jumamosi ya June 3, 2017 ni :-.
WALINDA MLANGO
Aley Ali Suleiman (Ubago) na Ali Makame (Muembe ladu)
WALINZI
Ibrahim Abdallah Hamad (Arahman), Abdurahman Seif Bausi
(Glorious), Abubakar Khamis (Bububu), Abdul aziz Ameir Khatib (Arahman), Ali
Issa Omar (Lumumba), Ahmed Mohd Shaaban
(Nyuki) na Abbas Yahya.
VIUNGO
Amani Ali Suleiman (Kiembe Samaki), Ibrahim Faraj “Mess”
(Lumumba), Haji Suleiman (JKU Mtoni), Yakoub Kiparo (Langoni), Jamali Ali Jaku
“Ozil” (Kinuni) na Eliyasa Suleiman (K-pura).
WASHAMBULIAJI
Faki Kombo (JKU Mtoni), Mundhir Abdallah (JKU Mtoni), Ali
Hassan (Bububu), Walid Abdi “Pato” (Mwera), Ali Mohd Seif (Tumekuja) na Ali
Omar (Mwera).
Comments
Post a Comment