JANG’OMBE BOYS HAO DAR KUWAFATA GOR MAHIA YA KENYA KWENYE SPORT PESA CUP
Timu pekee ya Zanzibar iliyopata nafasi ya kushiriki
Mashindano ya Sport Pesa Cup, Jang’ombe Boys wataondoka Visiwani Zanzibar kesho
majira ya saa 3 za asubuhi kuelekea Jijini Dar es salam tayari kwa mchezo dhidi
ya Gor mahia ya nchini Kenya mchezo ambao unatarajiwa kupigwa Jumanne ya June
6, 2017 saa 10:00 za jioni katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salam.
Kombe hilo ni la mtoano linashirikisha jumla ya timu nane , 4
kutoka Kenya, 3 Tanzania bara na 1 kutoka Visiwani Zanzibar.
RATIBA KAMILI HIYO
Jumatatu 5/6/2017
Singida united Vs FC leopard
Yanga Vs Tusker fc
Jumanne 6/6/2017
Simba Vs Nakuru All Star
Jang`ombe boys vs Gor mahia
Nusu fainali Alhamis
8/6/2017
Bingwa wa mechi kati ya Singida united vs AFC leopard
atacheza na bingwa kati ya Yanga na Tusker.
Nusu fainali ya pili Bingwa wa mechi kati ya Simba na Nakuru
all-star atacheza na bingwa wa mechi kati ya Jangombe boyz na Gor mahia
Fainali ni tarehe 11/6/2017 ambapo Bingwa wa SportPesa Super
Cup ataondoka na kitita cha dola 30,000 huku mshindi wa pili akipata dola
10,000.
![]() |
Jang'ombe Boys |
Comments
Post a Comment