JKU ACADEMY YAPANIA KUCHUKUA UBINGWA WA ROLLING STONE, MAPEMA WANATANGULIA ARUSHA KUZOWEA BARIDI

Timu za JKU Academy zimepania kubeba ubingwa wa Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati (Rolling Stone) ambapo mwaka huu wakitarajia kushiriki timu tatu tofauti katika Mashindano hayo ikiwemo timu chini ya miaka 13, 15 na 17 ambapo msafara wa watu 60 ukitarajiwa kuondoka Visiwani Zanzibar Jumapili usiku July 2, 2017.

Msafara huo ambao utajumuisha timu tatu tofauti za JKU Academy pamoja na waamuzi wao vijana watano na viongozi watano.

Mtandao huu umemtafuta Khatib Omar Salum ambae ni kocha mkuu wa JKU Academy na ametuelezea mchakato mzima wa safari yao kwenda huko na maandalizi yao walivyojipanga.

“Jumapili tunatarajia kuondoka Zanzibar, tunategemea Jumatatu tuanze safari ya Arusha na tutafika Jumatatu usiku, tunaenda mapema ili tuzowee mazingira ya baridi lakini pia mimi naamini tutabeba vikombe mwaka huu, tuna timu tatu n azote zipo vizuri sana mwaka huu”. Alisema.


Mashindano ya Rolling Stone mwaka huu yanatarajiwa kuanza rasmi July 9 na kumalizika July 19, 2017 ambapo msimu huu kumepangwa vituo tofauti makundi mengine yamepangiwa Arusha, mengine Manyara.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS