KANDA YA PEMBA NA UNGUJA ZAANZA VYEMA MASHINDANO YA UMISSETA MWANZA
Pazia la Mashindano ya Michezo na Sanaa ya Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA) limefunguliwa asubuhi ya leo huko Butimba Mkoani Mwanza kwa kuchezwa michezo mbali mbali.
Katika Mashindano hayo mwaka huu Zanzibar imeingiza kanda mbili tofauti, Unguja na Pemba ambapo kanda ya Pemba ikianza vyema michezo yake ya awali.
Kwa upande wa Soka Pemba wamefanikiwa kuondoka na alama 3 muhimu kufuatia ushindi wa bao 1-0 walipoichapa Manyara.
Bao pekee la Pemba limefungwa na Khamis Haji dakika ya 45.
Pemba wakaendelea kuwatesa Manyara sasa ni zamu ya Mpira wa Kikapu (Basketball) baada ya kushinda vikapu 64-21 dhidi ya Manyara.
Wakati huo huo kwa mchezo wa mpira wa Wavu (Volleyball) kanda ya Pemba ilianza vibaya kufuatia kufungwa na Mtwara seti 3-1.
Tukiachana na kanda ya Pemba pia kuna kanda ya Unguja ambayo pua inawakilisha Zanzibar katika Mashindano hayo ambapo mpaka sasa Unguja imecheza mchezo mmoja tu wa mpira wa Wavu na kufanikiwa kushinda seti 3-0 dhidi ya Katavi.
Kwa upande wa soka Unguja dhidi ya Katavi mchezo umeanza hivi punde saa 11:30, lakini endelea kufatilia blog hii utapata matokeo yote.
Mashindano hayo yote yanachezwa katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba mkoani Mwanza.
Comments
Post a Comment