“KILA MTU ANAWEZA NA HAKUNA KUKATA TAMAA HATA WAZANZIBAR WANAWEZA KUCHEZA LIVERPOOL” - MAMADOU SAKHO

Sakho na watoto wake akiwa pamoja na mmiliki wa blog hii Abubakar Khatib (Kisandu)
Katika Maisha hakuna kukata tamaa hasa kwa Vijana kwani hakuna kisichowezekana katika Dunia hii, hayo si maneno yangu bali ni maneno ya beki wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England wakati alipokuwa akiangalia mpira katika Visiwani Zanzibar katika Uwanja wa Aman kwenye mchezo maalum wa uzinduzi wa COCO SPORTS NDONDO CUP ambapo Taifa ya Jang’ombe walipigwa 2-1 na Mlandege.

Amesema ni kosa kwa kijana kukata tamaa kwani akiweka malengo na kujituma atatimiza ndoto zake.

“Ukiwa na malengo kisha ukajituma zaidi basi unaweza kutimiza ndoto zako, kwa wachezaji wa hapa Zanzibar hata Liverpool wanaweza kucheza lakini wakiwa na malengo yao na kujituma, hakuna kisichowezekana, mimi napenda kuona vijana hawakati tamaa”.

Aidha Sakho amefurahishwa mno katika mchezo huo kwenye uwanja wa Amaan huku akisema kuwa ame enjoy sana mapumziko yake Visiwani Zanzibar huku akisema mchezaji yoyote anaweza kucheza Ulaya.

“Nime enjoy sana Zanzibar, uwanjani mashabiki wengi wamenipokea kwa furaha na mimi nijisikia furaha sana, kuhusu wachezaji wa Zanzibar nimewaona lakini mimi maneno yangu ni yale yale, watu wote wanaweza kufanya lolote na kufika popote”.


Sakho ataondoka leo Saa 8 za mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume na kurejea nyumbani Ufaransa ambapo alikuwepo Visiwani Zanzibar na familia yake tangu Jumamosi ya June 17, 2017 kwa ziara ya kiutalii ambapo awali ziara hiyo alianzia Tanzania bara kisha kurejea nyumbani Ufaransa na badae moja kwa moja kufika hapa Zenj.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS