KOCHA BUSHIR, BARES, MALALE, NA MOROCO WAWAFUNGULIA NJIA NZURI MAKOCHA WA ZANZIBAR KWENYE LIGI KUU BARA, SASA WENGINE 4 WANAHITAJIKA
![]() |
Kocha wa Zanzibar Heroes Hemed Suleiman "Moroco" |
Idadi ya makocha kutoka Zanzibar kufundisha ligi kuu soka Tanzania
bara huenda ikaongezeka msimu huu mpya wa mwaka 2017-18.
Taarifa za uhakika tulizozinasa mtandau huu kuna makocha
wengne 4 huduma zao zinahitajika kwenye vilabu mbal mbali vya huko Bara.
Hayo yote yamekuja baada ya makocha wa kutoka Zanzibar msimu
ulopita kufanya vzuri katika ligi hiyo na kuziweka salama klabu zao kubakia
kwenye ligi hiyo.
Makocha hao wa Zanzibar waliyofundisha vilabu vya ligi kuu ya
bara na kuzisaidia timu zao kutoshuka daraja ni Ali Bushir Mahmoud “Benitez”
(Mwadui FC), Abdallah Mohammed Juma “Bares” (Prisons), Malale Hamsini Keya
(Ruvu Shooting) na Hemed Suleiman “ Morocco” (Stand United).
Zaidi endelea kufatilia Mtandao huu utapata kuwajua ni
makocha gani hao watakaopata shavu vilabu vya ligi kuu bara.
Mh sijapenda habari za uhakika kisha hamna majina wala timu zinazohitaji hao makocha uhakika ukowapi Kisandu kuwa makini
ReplyDelete