MAJERUHI YAIANDAMA UNGUJA, NYOTA WA 5 WA KIKOSI CHA KWANZA HUENDA WAKAIKOSA ROBO FAINALI LEO UMISSETA CUP
![]() |
Kikosi cha Unguja |
Timu ya Unguja inayoteremka Dimbani leo jioni kuwavaa wenyeji
Mwanza katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza kwenye mashindano
ya UMISSETA hatua ya robo fainali, imefikisha majeruhi 5 wa kikosi cha kwanza
ambao ni Mlinzi Abdul Azizi Ameir, viungo Haji Suleiman na Iliyasa Suleiman, na
washambuliaji Faki Kombo pamoja na Ibrahim Faraj “Mess”.
Wachezaji hao ambao ni nguzo kwenye kikosi hicho wana
asilimia kubwa kukosa mchezo huo baada ya kupata majeraha katika michezo yao ya
hatua ya makundi ikiwemo miwili ya jana ambapo mmoja walicheza asubuhi
wakaipiga Iringa 2-1 na mwengine walicheza jioni wakatoka sare na Dar es salam
2-2.
Kocha Mkuu wa kikosi hicho Mohammed Ally Hilaly “Tedy”
amekiri kuwa na majeruhi hao lakini bado anaimani timu yake itaibuka na ushindi
leo.
“Ni majeruhi ambao ndio nguzo katika timu, lakini bado
naimani ntashinda tu, ila Wazanzibar wajuwe kuwa mashindano hayo makugu sana,
mana leo tunacheza robo, tukishinda kesho tutacheza nusu nap engine kesho kesho
tutacheza fainali”. Alisema Tedy.
Comments
Post a Comment