MAJESHI WA TANZANIA WAPANIA KUFANYA KWELI MASHINDANO YA MAJESHI YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI


Timu za michezo mbali mbali za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zimepania kutwaa ubingwa katika Mashindano ya Majeshi ya Afrika Mashariki na Kati Mashindano ambayo mwaka huu yatafanyika Bujumbura Mjini Burundi mwanzoni mwa mwezi Agost.

Akizungumza na Mtandao huu Kanal Mwandike ambae ni Mkurugenzi wa Michezo wa JWTZ amesema wamepania kufanya kweli mwaka huu ambapo matayarisho ya Mashindano hayo yanaendelea vizuri na sasa wapo kambi Visiwani Zanzibar kwa kujiandaa na Mashindano hayo.

Amesema lengo lao mwaka huu kubeba kombe hilo ambapo mwaka jana walichukua nafasi ya pili katika Mashindano hayo.

“Mwaka huu tumepania kufanya vyema kuliko mwaka jana, mana mwaka jana tulishinda nafasi ya pili, tupo hapa Zanzibar kwaajili ya Maandalizi na tumepania kufanya kweli mwaka huu”. Alisema Kanal Mwandike.



Mashindano ya Majeshi ya Afrika Mashariki na Kati hufanyika kila mwaka, ambapo mwaka huu Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) litashiriki kwa michezo mitano ikiwemo mpira wa Miguu, mpira wa Kikapu, mpira wa Wavu, mpira wa Pete na Riadha.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS