MAMADOU SAKHO- “BABAANGU ALIKUFA NIKIWA NA MIAKA 12 NA MAISHA YALIKUWA MAGUMU MNO, SASA NINA UWEZO NA MUNGU ATANIULIZA PESA ZANGU NIMEZITUMIA VIPI? LAZIMA NIWASAIDIE WANYONGE


Sakho na familia yake wakipiga picha ya pamoja na watoto yatima wa SOS
Leo Saa 8 za mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ataondoka Beki wa kimataifa wa Ufaransa na kurejea nyumbani, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England ambae alikuwepo Visiwani Zanzibar tangu Jumamosi ya June 17, 2017 kwa ziara ya kiutalii ambapo awali ziara hiyo alianzia Tanzania bara kisha kurejea nyumbani Ufaransa na badae moja kwa moja kufika hapa Zenj.

Lakini mchezaji huyo anaondoka Zanzibar kwa kuwacha ujumbe mzito kwa Wazanzibar baada ya kusema kuwa yeye ni tajiri na anauwezo mkubwa sana lakini binafsi yake anajua fika kuwa akifariki Mwenyezi Mungu atamuuliza utajiri wake ameutumia vipi?

Amesema yeye anauwezo mkubwa wa fedha na muumini wa Dini ya Kiislamu hivyo Mungu atamuuliza fedha zake amezitumia kwa njia gani.
 
Watoto Yatima wa kituo cha SOS wakimsubiri Sakho katika kijiji chao Mombasa Unguja

“Mimi fedha ninazo nyingi sana na lakini najua fika kuwa Mungu ataniuliza nimezitumiaje fedha zangu!, nitamjibu vipi nimehonga wanawake!, hapana hivyo lazima nitowe sadaka kwa kuwasaidia watoto Yatima na Masikini na ndio maana nina taasisi yangu maalumu ya kusaidia Mayatima na Masikini”.

Wakati huo huo kumbe Sakho nae alikuwa mtoto yatima na aliishi maisha magumu sana wakati yupo mdogo na anajua umuhimu wa kuwasaidia mayatima ndio maana juzi akaenda kuwasaidia watoto Yatima wa kituo cha SOS Zanzibar.

Baadhi ya vyakula alivyotowa Sakho kwa Watoto Yatima

“Mimi babaangu mzazi alifariki nikiwa na miaka 12, nilikuwa mdogo sana na maisha yangu yalikuwa magumu sana, napenda kuwauliza wanangu AIDA (ana miaka 4) na SIENNA (ana miaka 2) mumezaliwa babaenu anaouwezo mkubwa wa mali kwaiyo na nyinyi mukiwa wakubwa fedha zenu mutafanya nini, basi wananiambia watasaidia masikini na Mayatima, nafurahi sana nikiwasikia hivyo na mimi nazidi kuwasisitiza wawasaidie”.

Sakho alikuwepo Zanzibar pamoja na mke wake anaitwa Majda ambae ana asili ya Moroco pamoja na watoto wao wawili wote wanawake ambao ni AIDA na SIENNA  waliozaliwa mwaka 2013 na 2015.

 
Sakho na mke wake (Majda) pamoja na watoto wake (AIDA na SIENNA)  

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS