MWINYI WA YANGA AWATAKA WACHEZAJI WA ZANZIBAR KUJITUMA ZAIDI ILI KUFANIKISHA MALENGO YAO, AKISISITIZA KUWA ZANZIBAR KUNA VIPAJI VINGI
Wachezaji wa soka Visiwani Zanzibar wametakiwa kuwa
wavumilivu, kuwa na nidhamu, pamoja na kufanya mazoezi kwa nguvu na bidii bila
kukata tamaa kama wanataka kufanikiwa malengo yao waliyojiwekea.
Wito huo umetolewa na mlinzi wa kushoto wa Yanga Mwinyi Haji
Ngwali “Bagawai” ambaye amewataka wanasoka hao hasa chipukizi kupenda kujifunza
na kuzingatia mafunzo ya walimu wao ili wafanikishe dhamira yao.
Mwinyi amesema Zanzibar kuna vipaji vingi sana na yeye
anawakubali Wazanzibar wenzake hivyo amewataka kuwa wavumilivu, nidhamu na
kujituma zaidi ili wafike wanapopataka.
Amesema ukicheza timu kubwa za Tanzania bara kama Yanga ndipo
utajua faida kubwa ya soka huku akiwasisitiza wachezaji wa Zanzibar wapigane
wafike Bara na kuona faina ya soka.
“Zanzibar kuna vipaji vingi sana tena mpaka utashangaa,
ukipita viwanjani utawaona watoto wanapiga soka hatari, mimi nawaomba wawe
wavumilivu, wawe na nidhamu, na wafanye mazoezi kwa nguvu na bidii bila kukata tamaa,
michezo inafaida nyingi sana, mfano mimi nimecheza Yanga miaka miwili tu basi
nimeona umuhimu wa soka, hakuna kisichowezekana, kwanini mimi nifike Yanga
wenzangu wa Zanzibar wasifike, mimi naamini kuna wachezaji wanauwezo zaidi ya
sisi tulofika hapa, lakini kubwa ndo hivyo hakuna kukata tamaa mazali bado upo
Duniani”. Alisema Mwinyi.
![]() |
Mwinyi Haji Ngwali “Bagawai” |
Comments
Post a Comment