PEMBA SOKA SIO SAFI UMISSETA, KESHO WANACHEZA TENA NA WENYEJI
Kikosi cha Pemba |
Wakiwa hawana tena matumaini ya kucheza nusu fainali na kwasasa wanakamilisha ratiba yao kwa michezo iliyosalia timu ya Soka ya Pemba kesho watacheza mchezo wao nne dhidi ya wenyeji timu ya Mwanza katika Mashindano ya Michezo na Sanaa ya Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA) katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba huko mkoani Mwanza.
Pemba walianza Mashindano hayo kwa matumaini makubwa katika mchezo wao wa awali baada ya kushinda 1-0 walipoichapa Manyara, baada ya hapo hawajashinda tena kufuatia mchezo wa pili kufungwa na Arusha 2-0, kisha wakafungwa tena Simiyu 2-1 na jana wakachapwa tena 2-1 na Kigoma, hivyo wamecheza michezo minne wameshinda mmoja tu na kufungwa mitatu.
Comments
Post a Comment