PEMBA SOKA WAMALIZA MECHI ZAO UMISSETA, WATOLEWA KATIKA MAKUNDI LAKINI WAMEMALIZA MECHI KWA FURAHA YA USHINDI
Kikosi cha Pemba |
Timu ya Soka ya Pemba leo imemaliza michezo yake yote ya
kundi “A” kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Tabora katika uwanja wa Chuo cha Ualimu
Butimba Mkoani Mwanza kwenye mashindano ya UMISSETA.
Katika kundi lao hilo “A” walikuwa pamoja na timu ya Manyara,
Simiyu, Arusha, Mwanza, Kigoma na Tabora ambapo wamecheza michezo 6 kwa
kushinda mechi 2, sare 1 na kufungwa 3 wakijikusanyia alama 7.
Wenzao Unguja bado ni kinara wa kundi “C” wakiwa na alama 15,
wakifukuzwa na Dar es salam wenye alama 13 wote wameshacheza michezo 5 na
lakini timu zote hizo mbili zimeshakata tiketi ya kucheza hatua ya robo
fainali.
Katika kundi hilo la Unguja lenye jumla ya timu 7 ambapo wapo
pamoja na Katavi, Kagera, Mara, Mbeya, Iringa na Dar es salam.
Michezo mitano ya awali Unguja waliifunga Katavi 4-0,
wakaichapa Kagera 3-0, juzi wakaipiga Mara 5-0, jana waituguwa Mbeya 1-0, na
leo wakaipiga Iringa 2-1, hivyo wameshafunga jumla ya mabao 15 katika michezo 5
waliyocheza wakati lango lao limeruhusu kufungwa bao moja tu.
Kikosi cha Unguja |
Comments
Post a Comment