PEMBA UTAIPENDA TU KWA BASKETBALL, YATINGA NUSU FAINALI, YAWATOA MABINGWA WATETEZI PWANI, WAPANIA KUBEBA KOMBE KWA MARA YA KWANZA
Kikosi cha Pemba Basketball |
Timu ya Mpira wa Kikapu (Basketball) ya Pemba imefanikiwa kutinga
hatua ya nusu fainali baada ya kuwatoa mabingwa watetezi timu ya Pwani kwa
vikapu 33-32 kwenye Mashindano ya Michezo na Sanaa ya Skuli za Sekondari
Tanzania (UMISSETA) katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba huko mkoani
Mwanza.
Pemba ikiwa mara yake ya kwanza kushiriki Mashindano hayo inaonekana
imepania kubeba Kombe hilo baada ya muendelezo mzuri kwa kushinda michezo yake
yote kwenye mashindano hayo.
Walianza kushinda vikapu 64-21 dhidi ya Manyara, kisha
wakaichapa Rukwa kwa vikapu 41-18 na leo kuwatupilia mbali mabingwa watetezi
Pwani kwa vikapu 33-32.
Sasa Pemba wanasubiri kucheza hatua ya Nusu fainali katika
mchezo huo wa Kikapu.
Comments
Post a Comment