RIPOTI YA KOCHA MALALE 50 YAJADILIWA LEO, ALIPENDEKEZA WACHEZAJI 10 KUACHWA NA KUSAJILIWA 6 RUVU SHOOTING
![]() |
Malale Hamsini Keya kocha wa Ruvu Shooting |
Mwenyekiti wa timu ya Ruvu Shooting, Kanali wa Jeshi na Mkuu
wa Kikosi cha Jeshi (CO) 832 Ruvu JKT, Charles Mbuge, leo asubuhi ameongoza
kikao cha viongozi wa timu kujadili taarifa ya Kocha Mzanzibar Malale Hamsini Keya
aliyoiwasilisha baada ya ligi (VPL) msimu wa mwaka 2016/17 kumalizika.
Katika taarifa yake, pamoja na mambo mengine, Mwalimu Malale
ameshauri wachezaji 10 kuachwa na wengine 6 kutoka klabu mbalimbali kuongezwa
ili kukiimarisha kikosi msimu mpya wa ligi 2017/18.
Comments
Post a Comment