UANACHAMA WA CAF UNAENDELEA KUFANYA KAZI ZAKE, TIMU ZA BEACH SOKA ZAPEWA MASHARTI
Na: Mossi Abdallah, Zanzibar.
Vilabu vya soka la ufukweni Zanzibar vilivyo shiriki ligi kuu
msimu uliopita vimepewa mwezi mmoja kuonana na mrajisi wa vyama vya michezo ili
kusajiliwa rasmi.
Akizungumza na Mtandao huu Fahad Khamis Said ambae ni katibu
wa kamati ya soka la ufukweni Zanzibar amesema vilabu hivyo wamevipa mwezi
mmoja vikafanyiwe uhakiki kwa mrajis.
Akisisitiza katibu huyo amesema timu yoyote ambayo haitaenda
kwa mrajis kuhakikiwa haitashiriki ligi kuu ya mchezo huo ambayo inatarajiwa
kuanza mwezi wa July mwaka huu kwenye
fukwe za Bububu Bambuu ambapo amesema kwakuwa Zanzibar imepata uanachama wa CAF
hawanabudi kufuta taratibu zote zilizokuwepo ili waendeshe kwa ufanisi zaidi
soka lao.
''Tumepata uanachama wa CAF kwaiyo kila kitu kiende kwa
utaratibu ikiwa timu haikwendwa kwa mrajis haitoshiriki ligi kuu msimu huu, bora
tuwe na vilabu saba lakini vimesajiliwa''. Alisema Fahad.
Comments
Post a Comment