UMISSETA ZANZIBAR WAMEREJEA NYUMBANI NA VIKOMBE 4
Zaidi ya Wanamichezo 134 kutoka Unguja na Pemba wamerejea
Visiwani Zanzibar mchana wa leo Jumamosi June 17, 2017 wakitokea Butimba Mkoani
Mwanza, kushiriki mashindano ya umoja wa Michezo na Sanaa skuli za sekondari
Tanzania (UMISSETA).
Akizungumza na Wanamichezo hao Bandarini Malindi Mjini Unguja
Naibu waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mmanga Mjengo
Mjawiri amewapongeza kwa kushindana katika mashindano hayo baada ya kurejea na
vikombe 4, moja cha mshindi wa kwanza na vitatu vya mshindi wa tatu.
“Kwa niaba ya Wizara ya Elimu Zanzibar nakupongezeni sana kwa
ushiriki wenu wa michezo kule Mwanza, na
pia nakupeni hongereni kwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu, sisi Wizara
tutaendelea na kuvitunza vipaji Mashuleni”. Alisema Mjawiri.
Mashindano hayo yaliyoanza June 6 na kumalizika juzi June 15,
2017 katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza ambapo Zanzibar
walifanikiwa kushinda nafasi ya kwanza kwa Wanaume kwenye mbio za Relay Mita 100
x 4, wakati kwa Mpira wa Kikapu, Wavu na mpira wa Mikono yote wakishika nafasi
ya 3.
Comments
Post a Comment