UNGUJA GUMZO MWANZA, NA LEO YA WAMPIGA MTU NYINGI, HAT TRICK KAMA KAWAIDA YAO
Timu ya soka
ya Unguja imeendelea kuwa gumzo jijini Mwanza kufuatia ushindi wake wa pili
mfululizo baada ya asubuhi ya leo kuwachapa Kagera mabao 3-0 kwenye Mashindano
ya Michezo na Sanaa ya Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA) katika uwanja wa
Chuo cha Ualimu Butimba mkoani Mwanza.
Nyota wa
mchezo huo ni Walid Abdi (Pato) alipiga hat trick na ndio bao lake la nne
katika Mashindano hayo kufuatia jana kufunga bao moja walipoichapa Katavi 4-0.
Huo ni
mwendelezo mzuri kwa vijana hao wa Unguja ambapo mpaka sasa wakiwa kinara wa
kundi lao C kwa alama zao 6 kufuatia kushinda michezo yote miwili na pia wana
jumla ya mabao 7 ya kushinda wakati lango lao linaloongozwa na Mlinda mlango
hatari Aley Suleiman “Manula” halijaruhusu kufungwa hata bao 1.
Pia katika
michezo hiyo miwili waliyocheza Unguja wameshafunga jumla ya Hat trick mbili
kufuatia leo Walid Abdi (Pato) kufunga na jana Mundhir Abdallah (Diarra)
kupiga.
Mchezo mwengine
Unguja watacheza na Mara Siku ya Jumamosi ya June 10, 2017, kisha kucheza tena Jumapili
June 11, 2017 dhidi ya Mbeya, Jumatatu June 12, 2017 Unguja dhidi ya Iringa,
Jumanne June 13, 2017 Unguja watamalizana na Dar es salam.
Unguja ndio
kinara akiwa na alama 6 wapo kundi “C” lenye jumla ya timu 7 ambapo wapo pamoja
na Katavi, Kagera, Mara, Mbeya, Iringa na Dar es salam.
KIKOSI CHA UNGUJA KILICHOPO MWANZA
KATIKA MASHINDANO YA UMISSETA
WALINDA MLANGO
Aley Ali
Suleiman (Ubago) na Ali Makame (Muembe ladu)
WALINZI
Ibrahim
Abdallah Hamad (Arahman), Abdurahman Seif Bausi (Glorious), Abubakar Khamis
(Bububu), Abdul aziz Ameir Khatib (Arahman), Ali Issa Omar (Lumumba), Ahmed Mohd Shaaban (Nyuki) na Abbas Yahya.
VIUNGO
Amani Ali
Suleiman (Kiembe Samaki), Ibrahim Faraj “Mess” (Lumumba), Haji Suleiman (JKU
Mtoni), Yakoub Kiparo (Langoni), Jamali Ali Jaku “Ozil” (Kinuni) na Eliyasa
Suleiman (K-pura).
WASHAMBULIAJI
Faki Kombo
(JKU Mtoni), Mundhir Abdallah (JKU Mtoni), Ali Hassan (Bububu), Walid Abdi
“Pato” (Mwera), Ali Mohd Seif (Tumekuja) na Ali Omar (Mwera).
Comments
Post a Comment