UNGUJA SOKA YATOA KIPIGO KIZITO MASHINDANO YA UMISSETA MWANZA
Timu ya soka ya kanda ya Unguja imeanza Mashindano ya UMISSETA kwa kishindo baada ya kuifumua Katavi mabao 4-0 mchezo uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza.
Mabao ya Unguja yamefungwa na Mundhir Abdallah (Diarra) akipiga hat trick na moja likifungwa na Walid Abdi (Pato).
Mchezo wao wa pili Unguja watacheza kesho dhidi ya kanda ya Kagera majira ya saa 4:00 za asubuhi katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba, Mwanza.
Comments
Post a Comment