UNGUJA YATINGA NUSU FAINALI BAADA YA KUWATOA WENYEJI MWANZA
Wenyeji wa Mashindano ya UMISSETA timu ya Soka ya Mwanza imeaga katika mashindano hayo baada ya kupigwa 2-0 na watoto wa Unguja, mchezo wa robo fainali uliosukumwa jioni ya leo katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba, Mwanza.
Mabao ya Unguja yamefungwa na Iliyasa Suleiman (Kotei) na Haji Sulieman(Van chaba).
Nusu fainali Unguja watasukumana kesho saa2 asubuhi dhidi ya Songwe katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba, Mwanza.
Comments
Post a Comment