WAJUWE MAKOCHA 7 WA ZANZIBAR WANAOENDELEA KUSOMA KOZI YA LESENI “A”
![]() |
Malale Hamsini Keya kocha wa Ruvu Shooting |
Ni jambo zuri na la kuvutia kwenye soka la Zanzibar linazidi kuengeza watu muhimu kwenye soka ambapo kesho Jumapili makocha (7) wa Zanzibar watakwenda kwenye kozi ya Makocha ya Leseni “A” inayotarajia kuendelea kesho kutwa Jumatatu ya June 12 na kumalizika June 29, 2017 katika ukumbi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Karume jijini Dar es salaam.
Makocha hao (7) ni Abdul mutik Haji “Kiduu” (Jamhuri),
Hababuu Ali Omar (JMK Youth Park), Abdallah Mohammed Juma “Bares” (Prisons),
Malale Hamsini Keya (Ruvu Shooting), Ali Vuai Shein (Kijichi), Salum Juma Makame (Tanga) pamoja na kocha
Salum Ali Haji (Chwaka Stars).
Kozi hiyo ni ya awamu ya pili baada ya kuanza July 17, 2016
na sasa wanaenda kumaliza sehemu ya pili na ya mwisho ambapo Mkufunzi Gwiji wa
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Sunday Kayun ndie anaefundisha kozi
hiyo.
Endapo makocha hao watafanikiwa kumaliza salama kozi hiyo,
idadi ya makocha wenye leseni “A” Zanzibar wataengezeka.
Kwa Zanzibar nzima makocha wawili tu
ndio wenye Leseni “A” ya ukocha wa shirikisho la soka barani Afrika (CAF) ambao
ni Hemed Suleiman Morocco kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar
Heroes) pamoja na kocha Nassra Juma ambae yeye ni kocha wa timu ya Taifa ya
Wanawake Zanzibar (Zanzibar Queens).
Kwa Tanzania nzima Nassra Juma ni mwanamke pekee mwenye leseni
ya juu ya ukocha ambapo ana leseni ‘A’ ya CAF na ‘B’ ya UEFA.
![]() |
Abdul mutik Haji “Kiduu” kocha wa Jamhuri |
Comments
Post a Comment