WALORATIBU SAFARI YA SAKHO WA LIVERPOOL ZANZIBAR 3:00 ZA ASUBUHI WATAZUNGUMZA NA COCONUT FM KUHUSU SAKHO KUFIKA AMAN LEO

Kampuni ya Escapade Zanzibar Limited ambayo ndio Kampuni iliyompokea na kusimamia shughuli zote za ziara ya Nyota wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England, Kampuni hiyo itazungumza na Coconut FM 88.9 leo kuanzia saa 3:00 za asubuhi na kumuelezea mchezaji huyo kuhusu ujio wake wa kwenda kuzindua Mashindano ya COCO SPORTS NDONDO CUP katika uwanja wa Amaan, mchezo ambao watasukumana kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Mlandege SC leo kuanzia saa 3:00 za usiku.

Sakho yupo hapa Viswani Zanzibar tangu Jumamosi June 17, 2017 kwa ziara ya kiutalii ambapo awali ziara hiyo alianzia Tanzania bara kisha kurejea nyumbani Ufaransa na badae moja kwa moja Jumamosi kufika hapa Zenj.

Wapenzi wa soka watakaofika katika Uwanja wa Amani leo watapata fursa ya kumuona na wengine kupiga nae picha nyota huyo.
Vingilio ni:-
Tsh 2000 urusi
Tsh 3000 wings

Tsh 5000 V.I.P

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS