WANAMICHEZO WA UMISSETA WAANZA SAFARI YA MWANZA ALAASIRI YA LEO, WATOA AHADI KWA WAZANZIBAR KURUDI NA VIKOMBE

Zaidi ya Wanamichezo 135 kutoka Unguja na Pemba wameondoka Visiwani Zanzibar alaasiri ya leo Jumamosi June 3, 2017 kuelekelea Butimba Mkoani Mwanza, kushiriki mashindano ya umoja wa Michezo na Sanaa skuli za sekondari Tanzania (UMISSETA).

Katika Mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Jumanne June 6, 2017 huko Butimba Chuo cha Ualimu Mkoani Mwanza, Zanzibar itakuwa na kanda mbili tofauti Unguja timu yao na Pemba timu yao, ambapo kanda ya Unguja itakuwa na timu za Soka, Wavu, Mikono, Riadha, Mpira wa Meza na Kikapu,wakati kanda ya Pemba itakuwa na timu za Riadha, Wavu, Kikapu na Soka.

Wanamichezo hao wameondoka  Zanzibar na boti ya Kilimanjaro 6 saa 9:30 Alaasiri kisha leo watalazimika kulala Dar es Salaam na wanatarajia kuondoka Dar es Salaam kesho Jumapili Juni 4 kwa mabasi maalum ya kukodi kuelekea Mwanza, ambapo watawasili Jumatatu Juni 5 siku ambayo timu zote zinatakiwa ziwe zimewasili.

Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE