WANAMICHEZO WA ZANZIBAR UMISSETA KUONDOKA KESHO KWENDA MWANZA
Zaidi ya Wanamichezo 135 kutoka Unguja na Pemba wanatarajia
kuondoka Visiwani Zanzibar kesho Jumamosi June 3, 2017 kuelekelea Butimba
Mkoani Mwanza, kushiriki mashindano ya umoja wa Michezo na Sanaa skuli za
sekondari Tanzania (UMISSETA).
Katika Mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua
vumbi lake Jumanne June 6, 2017 huko Butimba Chuo cha Ualimu Mkoani Mwanza, Zanzibar
itakuwa na kanda mbili tofauti Unguja timu yao na Pemba timu yao, ambapo kanda
ya Unguja itakuwa na timu za Soka, Wavu, Mikono, Riadha, Mpira wa Meza na
Kikapu,wakati kanda ya Pemba itakuwa na timu za Riadha, Wavu, Kikapu na Soka.
Wanamichezo hao wataondoka Zanzibar na boti ya jioni watalala Dar es
Salaam na wanatarajia kuondoka Dar es Salaam kesho kutwa Jumapili Juni 4 kwa
mabasi maalum ya kukodi kuelekea Mwanza, ambapo watawasili Jumatatu Juni 5 siku
ambayo timu zote zinatakiwa ziwe zimewasili.
Comments
Post a Comment