WAZANZIBAR WAIOMBEE DUA UNGUJA KUSHINDA LEO NUSU FAINALI

Timu ya Soka ya Unguja leo saa 3:00 za asubuhi itacheza nusu fainali dhidi ya Songwe katika Mashindano ya UMISSETA kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba  Mkoani Mwanza.

Unguja jana walifika hatua hiyo baada ya kuwatoa wenyeji Mwanza baada ya kuwafunga mabao 2-0 katika hatua ya Robo fainali.

Juzi Unguja walimaliza wakiwa wa kwanza katika kundi lao “C” baada ya kufikisha alama 16 kufuatia Michezo sita kucheza katika hatua ya makundi.

Katika michezo hiyo sita, michezo mitano wameshinda mfululizo na wa mwisho wametoka sare, awali Unguja waliifunga Katavi 4-0, wakaichapa Kagera 3-0, wakaipiga Mara 5-0, wakaituguwa Mbeya 1-0, na juzi asubuhi wakaipiga Iringa 2-1 na jioni wakatoka sare na Dar es salam 2-2, na jana wakawamaliza wenyeji Mwanza 2-0 kwenye hatua ya Robo fainali. 

Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE