BENDERA YA CAF HAIPO TENA ZANZIBAR MLINGOTI UPO MTUPU, MWENZAKE AMEFARIKI (BENDER
![]() |
Leo asubuhi katika uwanja wa Aman mlingoti wa Bendera ya CAF ukiwa mtupu |
Siku moja tangu Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kutangaza
kuifutia Zanzibar uanachama wake wa kudumu wa 55 wa Shirikisho hilo, leo kwa
mara ya kwanza Bendera ya CAF visiwani Zanzibar imeshindwa kupepea na kuambulia
mlingoti kuwa mtupu .
Tangu Zanzibar kupata uanachama wa shirikisho hilo Bendera ya
CAF ilikuwa ikipepea katika Uwanja wa Amaan sehemu ya V.I.P nje kwenye bustani
ndogo, na hiyo ilikuwa ni kiashiria ya kuwa kweli Zanzibar ni mwanachama wa
kudumu wa 55 wa shirikisho hilo.
Juzi Kamati ya utendaji ya CAF ilikutana mjini Rabat, Morocco
na kuamua mambo kadhaa likiwemo hilo la Zanzibar kufutiwa uanachama wake ambapo
Viongozi wakuu wa chama cha Soka Zanzibar (ZFA) walikuwepo katika Mkutano huo
ambapo alikuwepo Rais wa ZFA Ravia Idarous Faina, Katibu Mkuu wa ZFA Mohd Ali
Hilali “Tedy” pamoja na kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar
Heroes) Hemed Suleiman “Morocco”.
Jana Rais wa Caf, Ahmad Ahman amesema Zanzibar ilipewa nafasi
hiyo kimakosa na si sahihi kwa nchi moja kuwa na wanachama wawili wa shirikisho
hilo.
Zanzibar ilipewa uanachama wakati wa utawala wa Issa Hayatou
ambaye alikuwa akiungwa mkono na TFF chini ya Jamal Malinzi, hata hivyo Hayatou
aliangushwa na Ahmad Ahmad ambaye aliibuka mshindi katika uchaguzi wa CAF.
Hata hivyo, Zanzibar kuwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, imefanya kuvuliwa tena uanachama huo na kuendelea kubaki kama ilivyo.
Siku ya Alhamis Machi 16, 2017 itaendelea kukumbukwa na
Wazanzibar baada ya ZFA kuingizwa rasmi kuwa Mwanachama wa 55 wa Shirikisho la
Soka Barani Afrika “CAF” kufuatia Kikao cha 39 cha Mkutano Mkuu wa Shirikisho
hilo kilichofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia,uanachama ambao umedumu kwa
siku 128 tu tangu siku hiyo mpaka jana July 21, 2017.
Katika kura 54 za CAF, kura 51 zimekubali Zanzibar ipatiwe
uanachama wa kudumu wa Shirikisho hilo na nchi 3 zilikataa Zanzibar isipatiwe
ambazo ni Madagascar, Benin na Seychelles ambapo Madagascar ndio nchi anayotoka
Rais wa sasa wa CAF Ahmad Ahmad.
Comments
Post a Comment