DURU YA KWANZA LIGI KUU ZENJ INAANZA KESHO NA KUMALIZIKA JUMAMOSI, JKU NDIO KINARA, ANGALIA MSIMAMO HUU HAPA
![]() |
Kikosi cha JKU |
Mzunguko wa saba wa ligi kuu soka ya
Zanzibar hatua ya 8 bora utaanza kupigwa kesho Ijumaa 21/7/2017 kwa kupigwa
michezo mitatu ambapo mchezo nambari 25 Mwenge vs Taifa Jang’ombe saa 10 jioni
Gombani, Mchezo nambari 26 Jang’ombe boys vs Kizimbani saa 10 jioni Amaan na Mchezo
nambari 27 JKU vs Jamhuri saa 1:00 usiku Amaan.
Ligi hiyo itamaliza duru ya kwanza Jumamosi
22/7/2017 kwa Mchezo mmoja nambari 28 Okapi vs Zimamoto saa 10 jioni Gombani.
Mpaka sasa timu zote 8 zimeshacheza
michezo 6 ambapo katika msimamo JKU ndio kinara akiwa na alama 15 baada ya
kushinda michezo 5 na kupoteza mchezo 1 ambapo Jamhuri ikikamata nafasi ya 2
baada ya kushinda michezo 4, sare 1 na kupoteza mchezo 1 wakiwa na point 13
ambapo Jang’ombe Boys wanakamata nafasi ya 3 wakiwa na alama 13 baada ya
kushinda michezo 4, sare 1 na kupoteza mchezo 1 huku Zimamoto inakamata nafasi
ya 4 kwa alama zao 11 kufuatia kushinda michezo 3, sare 2 na kupoteza 1.
Nafasi ya 5 inakamatwa na Kizimbani
ambayo imeshinda michezo 2 na kupoteza michezo 4 wakiwa na alama 6 ambapo Okapi
akikamata nafasi ya 6 kwa point 5 baada ya kushinda mchezo 1, sare 2 na 3
kupoteza, wakati huo huo Taifa ya Jang’ombe inashika nafasi ya 7 kwa alama zake
3 kufuatia kwenda sare 3 na kupoteza 3 huku Mwenge akikamilisha nafasi ya 8
baada ya kwenda sare mchezo 1 na kupoteza michezo 5 akiwa na alama yake 1
pekee.
Ikumbukwe kuwa hatua hiyo ya 8 bora
ni kwaajili ya kuwatafuta Wawakilishi wa Zanzibar watakaoshiriki Mashindano ya
Kimataifa ambapo Bingwa atawakilisha kwenye Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika
na mshindi wa pili atawakilisha kwenye Kombe la Shirikisho Barani humo ambapo
msimu uliopita Zimamoto na KVZ waliwakilisha Zanzibar katika Mashindano hayo.
Comments
Post a Comment