FC MUEMBE BENI WAANZA VYEMA KUTETEA TAJI LAO CENTRAL LIGI, REAL KIDS HOI KWA SCHALKE 0
![]() |
FC Muembe Beni |
Mabingwa watetezi wa ligi za madaraja ya Vijana ndani ya
Wilaya ya Mjini kwa upande wa daraja la Central timu ya FC Muembe beni imeanza
vyema kampeni zake za kutetea taji lao baada ya kuifunga King Boys mabao 2-0 kwenye
mchezo wa 4 bora uliopigwa leo Jumapili July 9, 2017 kwenye dimba la Amaan saa
5 za asubuhi.
Mabao ya Muembe beni yamefungwa na Mselem Ali dakika 15 na
Othman Arafat dakika ya 89.
Mchezo mwengine umepigwa majira ya saa 7 za mchana ambapo Real
Kids watoto wa Kikwajuni wakafundishwa soka na watoto wa Muembe Makumbi ambao
ni Schalke 04 baada ya kufungwa mabao 2-1.
Mabao ya Schalke 04 yamefungwa na Iliyasa Suleiman dakika 6
na 18 wakati bao pekee la Real Kids limefungwa na Abdul halim Mohd dakika ya
39.
Comments
Post a Comment